Msukumo wa Jamii katika Mabadiliko ya Utendaji wa Tamthilia ya Kiswahili

Authors

  • Stella Faustine Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Tafiti mbalimbali zimekuwa zikijadili kuhusu tamthilia ya Kiswahili kwa kuangalia historia, maendeleo yake pamoja na vipengele vinavyounda utanzu huo kwa jumla. Vipengele vingine hasa vya mabadiliko ya utendaji wa tamthilia pamoja na msukumo wa kijamii katika kuzua mabadiliko hayo havikupewa kipaumbele. Hali hii imesababisha mabadiliko ya utendaji wa sanaa mbalimbali za maonyesho kama vile tamthilia, kutohusishwa na mabadiliko ya jamii, hivyo kusababisha ugumu katika kuelewa maudhui yaliyomo ndani yake kwa kina. Makala haya yanalenga kuziba pengo hilo kwa kuonesha namna msukumo wa jamii hususan uvumbuzi wa sayansi na teknolojia unavyochangia mabadiliko ya utendaji wa tamthilia. Makala yametumia data za maktabani ambazo zilipatikana kupitia njia ya udurusu wa nyaraka, mapitio ya tamthilia zilizohifadhiwa katika mfumo wa kidijiti, na usomaji makini wa tamthilia andishi. Data zilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli ambao hutumia maelezo katika uwasilishaji wa maudhui. Aidha, Nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti. Makala yamebainisha kuwa mabadiliko yaliyotokea katika jamii kama vile maendeleo ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, yana mchango mkubwa katika mabadiliko ya utendaji wa tamthilia. Kimsingi, makala yanatoa hamasa kwa waandishi na wahakiki wa tamthilia ya Kiswahili katika kuyahusisha maendeleo ya tamthilia na mabadiliko ya jamii

Downloads

Published

2021-08-17

Issue

Section

Articles