Tathmini ya Uwasilishaji na Upokezi wa Somo la Imla katika Shule za Upili nchini Kenya
Abstract
Makala haya yanalenga kutoa tathmini ya uwasilishaji na upokezi wa somo la imla katika shule za upili nchini Kenya. Somo la imla limeratibiwa kwenye mtaala na linapaswa kufundishwa kuanzia shule za msingi hadi za upili (KIE, 2005). Somo hili ni mojawapo ya masomo katika stadi ya kuandika. Ufundishaji wa somo la imla unapaswa kuimarisha vipengele vya stadi ya kuandika lakini kwa mujibu wa utafiti wa awali uliofanywa suala hili linasailika. Wanafunzi katika shule za upili bado wanafanya makosa mengi ya tahajia, uakifishaji, msamiati, matamshi na sarufi ambayo yanapaswa kupunguzwa au kuondolewa kabisa na masomo katika stadi ya kuandika hasa somo la imla. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa ufundishaji wa somo la imla unaathiri stadi ya kuandika na matumizi ya lugha kwa jumla. Hata hivyo, somo la imla linaonekana kuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha stadi ya kuandika na kuzungumza ikiwa litafundishwa ipasavyo. Kwa hivyo, makala haya yanatalii somo la imla kwa undani kwa lengo la kubainisha umuhimu, uwasilishaji na upokezi wake na kutathmini ikiwa kuna udhaifu unaofanya malengo ya somo hili yasiafikiwe katika kazi za wanafunzi wa shule za upili nchini Kenya. Makala haya pia yanatoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha uwasilishaji na upokezi wa somo la imla nchini Kenya.