Changamoto za Tafsiri katika Enzi ya Utandawazi
Abstract
Ulimwengu unaendelea kuwa mdogo kwa sababu ya utandawazi. Katika muktadha wa lugha na fasihi ya Kiswahili, tunaweza kusema kuwa utandawazi umekuwa na athari kubwa kifasihi, kiisimu na kijamii. Ulimwengu wa sasa umeshuhudia ongezeko la matumizi mapana ya lugha anuwai za ulimwengu mbali na Kiingereza. Lugha kama Kiswahili, Kihindi, Kimandarin, Kichina, Kirusi, Kifaransa, Kiarabu na Kijapani zimeshuhudia ongezeko la matumizi yake kutokana na utandawazi. Kwa sababu hii, wafasiri na wakalimani walio na ujuzi katika lugha hizi wanahitajika katika maeneo anuwai ya ulimwengu. Hii ni kusema kuwa utandawazi umesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za tafsiri. Mbali na kupanuka kwa matumizi ya lugha, mahitaji haya pia yamesababishwa na teknolojia mpya ambayo imesababisha kupungua kwa gharama ya kubadilishana kwa ujumbe na matokeo ya tafiti. Changamoto za kisiasa ulimwenguni nazo zimesababisha haja ya kuwapo kwa wafasiri na wakalimani wengi katika kila pembe ya ulimwengu ili kushirikishwa katika michakato ya kutafuta amani na mapatano. Kwa sababu hii, changamoto anuwai zimezuka na kukumba wafasiri ikiwamo michakato ya tafsiri na vifaa vinavyotumika kutekeleza jukumu hili. Makala haya yanajadili changamoto zinazowakumba wafasiri katika michakato yao ya kutafsiri matini mbalimbali enzi au zama za sasa, zama za utandawazi.Downloads
Download data is not yet available.