Upenyezaji na Ukubalifu wa Mkururo wa Konsonanti katika Fonolojia ya Kiswahili: Mifano katika Maneno Yaliyopokelewa kutoka Kiingereza na Kiarabu

Authors

  • Majariwa David Idara ya Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu Kabale, Uganda

Abstract

Ikisiri

Makala haya yanachunguza jinsi mikururo ya konsonanti [Skr-]/[Sk-], [Spr-]/[Sp-], na [Str-]/[St-] ilivyopokelewa katika fonolojia ya Kiswahili kutoka Kiarabu na Kiingereza. Lengo kuu ni kuelezea jinsi mikururo hiyo ya konsonanti ilivyopenyeza na kukubalika katika mfumo wa fonolojia ya Kiswahili. Mifumo ya fonolojia ya lugha inafikiriwa kuwa thabiti zaidi dhidi ya mabadiliko ikilinganishwa na nyanja nyingine za isimu. Data zilizotumika zilipatikana kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) (2013), Toleo la Tatu pamoja na Bosha (1993). Mbinu ya orodhahakiki na usomaji nyaraka zilitumiwa kupata data. Nadharia ya Umbo Upeo ilitumiwa katika uchanganuzi wa data. Uchopezi wa irabu ni mkakati unaozingatiwa sana wakati wa urekebishaji wa mkururo wa konsonanti katika maneno yanayopokelewa katika Kiswahili (Mwita, 2014; Akidah, 2013). Hata hivyo, imebainika kuwa mikururo wa konsonanti [Skr-]/[Sk-], [Spr-]/[Sp-], na [Str-]/[St-] ilighairi mikakati ya urekebishaji na kupenyeza katika fonolojia ya Kiswahili. Upokeaji wa mikururo hiyo ya konsonanti uliwezekana kupitia upangiliaji upya wa mashartizuizi ya Kiswahili. Upangiliaji wa mashartizuizi ulichochewa na haja ya kuwa na uwekevu wa nguvu katika utamkaji. Hivyo, ukubalifu wa mikururo ya konsonanti umeelezwa kupita wepesi wa utamkaji uliochochea upangiliaji wa mashartizuizi ya mfuatano wa konsonanti katika Kiswahili.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2022-04-16

Issue

Section

Articles