Ulinganishi wa Mfumo wa Ngeli za Nomino katika "Lugha" za Kibantu za Mara Kaskazini

Authors

  • Alphonce B. Morango Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Ikisiri

Makala haya yanahusu uchunguzi wa mfumo wa ngeli za nomino katika "lugha[1]" zilizo Kaskazini mwa mkoa wa Mara ambazo ni Kikurya, Kisimbiti, Kikiroobha, Kisweeta, Kikabwa, Kisuba1, Kikine na Kikenye. Mkoa huu una lugha nyingi ambazo zinafanana, ingawa wazungumzaji wake wanadai wanazungumza lugha tofauti. Makala haya yanachunguza mfanano na tofauti za mfumo wa ngeli katika "lugha" za Kibantu za Mara Kaskazini. Nadharia inayoongoza uchunguzi wa mfumo huu ni "Nadharia ya Isimu Historia-Linganishi" iliyoasisiwa na mwanaisimu William Jones (1786). Msisitizo mkubwa wa nadharia hii ulikuwa kulinganisha lugha kwa lengo la kufanya uundaji upya wa lugha ya awali. Data zilizotumika katika makala haya zimepatikana kutoka uwandani, ambapo wazungumzaji wa lugha hizo wanapatikana. Utafiti ulitumia mbinu za kusikiliza, usaili, hojaji na majadiliano kwenye majopo katika ukusanyaji wa data. Aidha, mbinu ya kikompyuta ilitumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwa kuna mfanano mkubwa wa "lugha" hizi wa takribani asilimia sabini na saba (77%). Hivyo, hizi si lugha zinazojitegemea bali ni lahaja ambazo zimetokana na lugha moja kuu ya awali na kugawanyika katika makundi mawili: kundi moja linahusisha Kikurya, Kisimbiti, Kikiroobha, Kisweeta, Kikine, na Kikenye. Kundi la pili lina lugha za Kisuba na Kikabwa

[1]Neno lugha linapoandikwa kurejelea lugha za Mara Kaskazini linawekewa funga na fungua semi     (" ") kwa sababu lugha hizi haziko bayana kama ni lugha zinazojitegemea au ni lahaja za lugha moja kuu ya awali. Hii inatokana na mfanano uliopo katika lugha hizi. Mfanano huo ndio unaosababisha msigano miongoni mwa wanaisimu na wanajamii ambapo baadhi wanadai ni lahaja tu za lugha moja na wengine wanadai ni lugha zinazojitegemea, kwani katika jamii hizi kila kabila hujinasibu na lugha yake, ikiiona kuwa iko tofauti na jamii nyingine.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2022-04-16

Issue

Section

Articles