Uchunguzi wa Umajumui na Umahususi wa Nduni za Shujaa wa Kiafrika katika Kisakale cha "Mukwavinyika"
Abstract
Ikisiri
Makala haya yanalenga kufafanua usawiri wa nduni za shujaa katika kisakale cha "Mukwavinyika." Tafiti mbalimbali zilizofanywa kuhusu ujitokezaji wa nduni za shujaa wa Kiafrika katika tanzu anuwai za kifasihi zimethibitisha kuwa mashujaa wa Kiafrika wana nduni zilizo karibu sawa, yaani kwa kiasi kikubwa zinafanana (taz. Johnson, 1986; Mulokozi, 1999; Mahenge, 2016; Kazinja, 2017; Mtega, 2017, na Sosoo, 2018). Maelezo ya wataalamu hawa yanadhihirisha kuwa nduni za mashujaa duniani kote zinafanana na ni za kimajumui. Makala haya yanadadisi umajumui wa nduni hizo na kuzidi kuhoji kuwa kwa kuwa fasihi ni zao halisi la jamii mahususi, hivyo, zaidi ya kuwa na sifa za kimajumui, mashujaa wana sifa mahususi kulingana na jamii husika. Hivyo, makala haya yamefafanua umajumui na umahususi wa nduni hizo za shujaa wa Kiafrika huku yakimtumia Mukwavinyika wa jamii ya Wahehe kama mfano wa mashujaa hao.