Tathimini ya Matumizi ya Lugha ya Kiingereza katika Kuendesha Mashauri Mahakamani Nchini Tanzania

Mwinyikombo Ally Mwinyikombo

Abstract


Ikisiri

Makala haya yanalenga kuainisha na kutathmini athari zilizopatikana kutokana na matumizi ya lugha ya Kiingereza katika uendeshaji wa mashauri mahakamani nchini Tanzania. Matumizi ya lugha hii ni urithi ambao mahakama iliuenzi tangu baada ya uhuru mwaka 1961 mpaka mwaka 2021 Kiswahili kiliporasmishwa kuwa lugha ya sheria na mahakama. Lugha ya Kiingereza ilikuwa ikitumika tangu enzi ya ukoloni katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na  uendeshaji wa mashauri mahakamani. Hata hivyo, uzoefu unaonesha kuwa kutawaliwa siyo kigezo cha matumizi ya lugha ya mtawala katika uendeshaji wa mashauri katika mahakama, kwani zipo nchi ambazo katika utoaji haki hazitumii lugha zilizokuwa zikitumiwa na watawala wao. Mjadala kuhusu matumizi ya lugha ya Kiingereza katika makahama unachagizwa na ukweli kwamba, Kiswahili ni lugha rasmi na ya taifa nchini Tanzania. Hivyo, ni dhahiri kwamba matumizi ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mahakama yatasaidia kurahisisha mawasiliano na utoaji wa haki katika jamii ambayo huitumia lugha hii kwa kiasi kikubwa katika mawasiliano yao ya kila siku.  Data za utafiti uliozaa makala haya zilikusanywa kwa njia ya hojaji na usaili. Makala haya yamegawanyika katika sehemu nane ambazo ni utangulizi, mapitio ya machapisho kuhusu kumea kwa lugha ya Kiingereza nchini Tanzania, mbinu za utafiti, sababu za matumizi ya Kiingereza mahakamani, madai ya Kiswahili kutumika mahakamani, athari za matumizi ya Kiingereza mahakamani, mapendekezo na hitimisho.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.