Mfumo Faafu wa Ukonganyaji Istilahi za Sayansi na Teknolojia katika Kiswahili

Zabron T. Philipo

Abstract


Ikisiri

 

Makala haya yanaonesha mfumo faafu wa ukonganyaji Istilahi za Sayansi na Teknolojia (kuanzia sasa IST) katika Kiswahili. Uundaji wa istilahi hususani katika lugha ya Kiswahili umeonekana kutilia mkazo zaidi katika mtazamo wa ukonganyaji istilahi mahususi. Mtazamo unaosisitiza ukusanyaji istilahi kwa ajili ya uundaji istilahi kutokana na mwitikio wa wanaistilahi kutaka kuunda istilahi mpya. Pia, ukonganyaji huu ni ule wa kuandaa kongoo ya istilahi kwa ajili uundaji istilahi. Hoja na mifano zilikusanywa kutokana na usomaji wa nyaraka hususani, nyaraka za BAKITA (Istilahi za Kiswahili) na TATAKI (Kamusi Sanifu Biolojia Fizikia na Kemia) na usaili. Hoja na mifano hiyo zinahalalisha umakinikiaji wa ukonganyaji istilahi katika lugha ya Kiswahili. Makala haya yanajikita katika mtazamo wa ukonganyaji istilahi tarakibishi. Mtazamo unaosisitiza kanuni tatu za kuzingatia; mosi, ukusanyaji istilahi wa kongoo; pili, ukusanyaji wa kanzidata ya istilahi na taarifa husianifu yaani, kwa lengo la kuanzisha benki ya istilahi au utunzi wa kamusi ya istilahi za kiufundi; na tatu, ukusanyaji istilahi wa uendelezaji stahilifu. Lengo la ukonganyaji istilahi kwa mkabala huu ni kuwa na uundaji wa istilahi  unaokidhi haja ya mawasiliano mahsusi katika nyanja husika. Hivyo, ukonganyaji huu utarekebisha ukonganyaji uliopo sasa na kuwa na mfumo bora wa ukonganyaji istilahi za fani mbalimbali katika lugha ya Kiswahili.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.