Maarifa ya Jadi katika Fasihi ya Kiswahili: Uchunguzi kutoka Riwaya ya Wacha Mungu wa Bibi Kilihona

Lameck E. Mpalanzi

Abstract


Maarifa ya jadi ni taaluma muhimu katika mfumo wa maisha ya Mwafrika tangu kale. Mahali pengi Afrika, maarifa ya jadi hutazamwa kama maarifa yanayopatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu. Makala haya yanalenga kubainisha masuala ya epistemolojia[1] ya Kiafrika kwa kutumia mifano kutoka riwaya ya Wacha Mungu wa Bibi Kilihona. Vilevile, makala yanafafanua dhima za maarifa hayo kwa jamii. Hivyo, makala haya yanajenga hoja kwamba fasihi ya Kiswahili ina maarifa faafu yanayoongoza maisha ya Waafrika tangu kale. Hoja hii inapinga mtazamo wa baadhi ya wanazuoni wa Kimagharibi akiwamo Hegel (1975) wanaodai kwamba Afrika ni bara giza lisilo na maarifa, ustaarabu wala maendeleo. Makala yanawachagiza wanazuoni na Waafrika kwa ujumla kuyaonea fahari maarifa yao. Katika kukamilisha malengo haya, Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika imetumika katika kuhakiki maarifa ya jadi na kufafanua dhima za maarifa hayo kwa jamii. Mbinu zilizotumika katika uchambuzi na uwasilishaji data ni uchunguzi, udurusu wa maandiko maktabani na usomaji makini. Makala haya yamebaini kuwa riwaya ya Kiswahili hubeba maarifa ya jadi yanayowatambulisha Waafrika. Maarifa hayo huaminika kutatua matatizo yao kama yatatumika kwa ukamilifu wake. Makala yanahitimishwa kwa kueleza changamoto na mapendekezo mahususi.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.