Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania

Authors

  • Fokas Nchimbi Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa

Abstract

Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la makala haya ni kuonesha maeneo muhimu ya uchaguzi ambamo lugha ya Kiswahili inatumika, na kupendekeza mikakati inayoweza kufanikisha lugha hiyo kutumika zaidi katika masuala ya uchaguzi na kwenye michakato mingine ya ujenzi wa demokrasia Tanzania. Makala haya yanaakisi matumizi na mchango muhimu wa lugha ya Kiswahili katika michakato ya siasa za uchaguzi nchini Tanzania kama sehemu ya ujumuishaji wa kidemokrasia. Inaonesha kuwa katika michakato ya uchaguzi nchini Tanzania, lugha ya Kiswahili inatumiwa ili kufanya mawasiliano yanayoweza kuwajumuisha Watanzania wengi kwenye hatua mbalimbali za shughuli za uchaguzi. Makala haya yanatumia Nadharia ya Uchambuzi Kilongo. Nadharia hii inaeleza kuwa athari za matumizi ya lugha hazibaki kwenye eneo lake la matumizi pekee bali huvuka mipaka ya muktadha wa matumizi yake na kuathiri masilugha mengine. Makala haya yametumia data za upili ambapo nyaraka ngumu na laini zilizoandikwa kwa Kiswahili kuhusu shughuli za uchaguzi nchini Tanzania zilisomwa. Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti uliozaa makala haya yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inawawezesha Watanzania wengi kujumuishwa kwenye demokrasia ya uchaguzi kupitia michakato mbalimbali ambayo ni uandikaji wa matini tumizi ya uchaguzi, nyimbo za kampeni za uchaguzi, utangazaji wa matokeo ya uchaguzi, uapisho wa viongozi wateule, uandikaji wa ripoti ya uchaguzi na tathmini ya uchaguzi. Makala haya yanapendekeza kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yaimarishwe zaidi kwenye michakato ya uchaguzi na kwenye michakato mingine ya kisiasa ili kujenga ujumuishi mpana wa kidemokrasia.

Downloads

Download data is not yet available.

Author Biography

Fokas Nchimbi, Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa

Mwalim

Downloads

Published

2023-03-21

Issue

Section

Articles