Utendaji wa Wahusika Wakuu wa Fasihi ya Watoto ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Ngoma ya Mianzi
Abstract
DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na42t1.3Makala haya yanayohusu utendaji wa wahusika wakuu wa fasihi ya watoto ya Kiswahili ni sehemu ya utafiti uliofanywa kwa ajili ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Data za utafiti zilipatikana uwandani na maktabani kwa kusoma riwaya teule na kufanya usaili na mwandishi wa riwaya hiyo na wataalamu wa fasihi ya watoto. Data hizo zilichanganuliwa kwa mbinu ya kimaudhui kwa sababu utafiti ulikuwa wa kitaamuli. Nadharia ya Saikochanganuzi ya Sigmund Freud (1856-1939) ilitumika katika uchanganuzi huo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa utendaji wa wahusika wakuu unaweza kudhihirika kwa mtindo wa kuhoji, kutaarifu, kushauri, kudadisi na kuonya. Mtindo huu umebainika kutokana na mazungumzo baina ya wahusika na masimulizi ya kiutendaji yanayokwenda sambamba na mazungumzo hayo. Kwa mujibu wa Mbunda (1993), lugha ya mazungumzo huwekwa katika riwaya ili isimchoshe msomaji, ambaye katika muktadha wa makala haya, ni mtoto wa miaka 15 hadi 18. Mtafiti anapendekeza watunzi, wahakiki na wataalamu wa kazi za fasihi, hususani fasihi ya watoto kutafiti mitindo hii katika riwaya nyingine za watoto.