Tathmini ya Anthropomofiki katika Riwaya ya Shamba la Wanyama

Waithiru Kago Antony, Sheila Wandera-Simwa, Onyango Ogola James

Abstract


DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na42t2.5

 

 

Makala haya yanatathmini namna anthropomofiki ilivyotumika katika riwaya ya Shamba la Wanyama ya George Orwell. Orwell ni miongoni mwa waandishi maarufu na waliosifika katika fani na utunzi wa kazi za fasihi zinazokashifu mfumo wa utawala wa kibepari, kwa kutumia mbinu ya anthropomofiki. Lengo kuu la makala haya ni kujadili jinsi ambavyo anthropomofiki imetumiwa na mwandishi katika kukabiliana na ubepari ulimwenguni. Hivyo, makala haya yanajikita katika kujadili mapinduzi yaliyozalishwa na elimu na yaliyowasilishwa kianthropomofiki na George Orwell. Katika kufanikisha tathmini hii, makala haya yaliongozwa na baadhi ya mihimili mikuu ya nadharia ya Uhakikimazingira kama ilivyoasisiwa na Glotfelty, Fromm pamoja na Buell. Mihimili miwili mikuu iliyoongoza tathmini ya makala haya ni uwezo na kifo, na uongozi mbaya na ukoloni mamboleo. Nadharia hii imejikita katika uhakiki wa matini za kifasihi kwa kudhihirisha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Data ya makala haya ilipatikana maktabani. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mwandishi amefanikiwa kukemea ubepari kupitia mbinu ya anthropomofiki katika riwaya teule. Riwaya hii iliteuliwa kwa kudhamiria kutokana na kuwepo kwa suala la mazingira ya binadamu kupitia mbinu ya anthropomofiki.


Full Text:

217-237

Refbacks

  • There are currently no refbacks.