Nafasi ya Lugha katika Elimu Barani Afrika: Suala la Kiswahili na Lugha zingine za Kijamii nchini Tanzania

Martha A. S. Qorro, Philpo John

Abstract


DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na42t2.1

 

Makala haya yamejenga hoja juu ya kwa nini lugha ya Kiswahili na lugha zingine za Kiafrika zipewe hadhi stahiki katika mifumo ya elimu Barani Afrika, hususani Tanzania. Makala yamedadavua kwa kina jinsi ambavyo matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya msingi, sekondari na kuendelea yanaweza kuleta athari chanya katika mfumo wa elimu nchini Tanzania na namna ambavyo matumizi ya lugha zingine za asili katika madarasa ya awali nchini yanaweza kujenga msingi imara kwa mtoto. Data za makala haya zimepatikana kutoka katika matini za maktabani ambazo kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita zimethibitisha kwamba matumizi ya lugha ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya sekondari yameendelea kuleta athari hasi katika mfumo wa elimu nchini Tanzania. Makala haya yameonesha jinsi ubeberu wa lugha unavyoiathiri jamii husika kiutamaduni na kiuchumi; na jinsi ambavyo tunaweza kujikomboa kutoka katika mtego huu uliotegwa na watawala wa kikoloni kupitia lugha zao. Pia, makala haya yameeleza kwa kutumia Nadharia za Ujifunzaji Lugha jinsi lughamama inavyopaswa kuweka msingi imara katika madarasa ya awali ili mtoto aweze kumudu kujifunza Lugha ya Pili na zingine zinazofuata. Makala yamehitimisha kuwa matumizi ya lugha ya kigeni kama Kiingereza nchini Tanzania, kwa mfano, yameendelea kuiathiri elimu ya sekondari na kuendelea. Hivyo, hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kujikomboa na mtego huu wa utawala wa kifikra na kiutamaduni kupitipia ubeberu wa lugha. Makala yametoa mapendekezo nane yanayoweza kusaidia kufikia lengo la kujikomboa.


Full Text:

139-163

Refbacks

  • There are currently no refbacks.