MTINDO WA JAZANDA KATIKA TAMTHILIA YA KIJIBA CHA MOYO

Sophie Nyehita Okwena

Abstract


Makala haya yanashughulikia jazanda zilizomo katika tamthilia ya kifalsafa ya Kijiba cha Moyo (2009) iliyotungwa na Timothy Arege. Msuko wake unashabihiana na ule wa Mashetani (1971), tamthilia ya kifalsafa ya Ebrahim Hussein. Tathmini hii inaongozwa na nadharia ya kimtindo. Tumeteua kuhakiki tamthilia hii kwa msingi kwamba ni tamthilia ambayo imeandikwa kwa falsafa ya kiwango cha juu na inasheheni lugha fiche ya jazanda. Jazanda ni miongoni mwa vipengele muhimu vya lugha hivyo, matumizi mwafaka yanadhihirisha umahiri wa mtunzi. Kwa upande mwingine, matumizi chapwa ya jazanda yanaweza kuleta utata na kupotosha ujumbe wa mtunzi. Jazanda zinatumika kuleta uangavu, mvuto, ubora na utofauti wa kipekee katika kazi ya mtunzi. Aidha, jazanda ni mbinu kwasi ya usanii na mtunzi anayeitumia hufanikisha uandishi wake kwa kuendeleza maudhui na kukuza wahusika wake. Watunzi wengi hutumia jazanda kuwasilisha tajriba zao, mawazo yao na hisia zao katika vipindi na wakati wao. Kwa hiyo, sharti kuwe na uwiano kati ya ujumbe wa mtunzi na jazanda ambazo ametumia kwa sababu jazanda  inapotumika katika njia mwafaka huchangia katika ufanisi wa kazi ya kisanaa kwani hutumiwa katika uzuaji na ubunifu wa kifasihi.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.