TATHMINI YA MAANA KATIKA MANENO AMBATANI YA KISWAHILI

Authors

  • Katikiro G. Katikiro University of Dar es salaam

Abstract

"Neno ambatani" ni neno linaloundwa kwa kuambatanisha maneno mawili au zaidi ili kuunda neno moja linalorejelea dhana au kitu kimoja. Semantiki ya neno ambatani ni jambo ambalo wachunguzi wengi wameliweka kando. Tafiti nyingi zinachukulia kuwa maana ya neno ambatani haitokani au haiwezi kuashiriwa na maneno ya asili yanayounda neno ambatani husika (Rubanza, 1996:113). Mtazamo huu wa kuona kuwa maana ya neno ambatani haiwezi kutokana na viambajengo vyake unaweza kusailiwa. Kwa hiyo, makala hii inachambua maana za maneno ambatani katika Kiswahili ili kubainisha mchango wa maana za manenojenzi katika maana tokeo ya neno ambatani.   Aidha, makala hii inatathmini nafasi ya maana katika uundaji wa maneno ambatani ya Kiswahili.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-04-11

Issue

Section

Articles