Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza

Authors

  • Rehema Julius Magembe Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira
  • Perida Mgecha Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira

Abstract

Makala haya yanalinganisha uingizaji wa vidahizo homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la nne (KKS4) (2004) na Kamusi la Kiswahili Fasaha toleo la kwanza (KKF1) (2010). Malengo mahususi ya makala haya ni kueleza tofauti na ufanano unaojitokeza katika uingizaji wa vidahizo homonimu baina ya kamusi hizo mbili. Mbinu ya uchambuzi matini imetumika kupata data za makala haya. Makala haya yameongozwa na Nadharia ya Metaleksikografia iliyoasisiwa na Weigand (1984). Matokeo yanaonesha kuwa kuna tofauti katika uingizaji wa vidahizo homonimu baina ya KKS4 na KKF1 ambazo zimejidhihirisha katika taarifa za kimatamshi, kietimolojia, uhusika wa vitenzi pamoja na uingizaji wa fasili za maana. Baadhi ya tofauti zinasababishwa na tofauti za kiutamaduni na maeneo ya kijiografia baina ya watumiaji wa kamusi teule ambamo lugha ya Kiswahili inatumika. Hata hivyo, makala haya yamedhihirisha kuwapo kwa ufanano wa uingizaji wa vidahizo homonimu katika KKS4 na KKF1 katika vipengele vya tahajia, matamshi, ubainishaji wa viambishi vya umoja na wingi pamoja na ubainishaji wa viambishi vya upatanisho wa kisarufi. Kwa ujumla, taarifa zilizoingizwa katika KKS4 ni nyingi kuliko taarifa zilizoingizwa katika KKF1. Hivyo, ni vyema kushughulikia katika matoleo yanayofuata ya kamusi hizi teule yale yanayoonekana kuwa ni tofauti zenye changamoto ili kuwa na kamusi zenye utoshelevu zaidi.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.2

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-06-30

Issue

Section

Articles