Ujitokezaji wa Mbinu za Kibalagha katika Hotuba za Dkt. Samia Suluhu Hassan

Authors

  • Ahmad Y. Sovu Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Abstract

Balagha ni mbinu za matumizi ya lugha ambazo mzungumzaji huzitumia ili anachokiwasilisha kiwashawishi au kuwafurahisha wasikilizaji (TUKI, 2013). Kwa kawaida, uwasilishaji huo hufanywa kwa njia ya maandishi, mazungumzo, picha na kadhalika (Lupogo na Ambrosi, 2023). Shabaha ya makala haya ni kuonesha ujitokezaji wa mbinu za kibalagha katika hotuba za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (kuanzia sasa Samia), ili kushawishi na kufikisha ujumbe ulioukusudiwa kwa hadhira. Data za makala haya zimekusanywa maktabani kwa kupitia maandiko na pia uwandani kwa kuwahoji wanataaluma mbalimbali. Uchambuzi na uwasilishaji wa data za makala haya umeongozwa na Nadharia ya Balagha. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kuwa katika hotuba zake, Samia hutumia mbinu mbalimbali za kibalagha. Miongoni mwa mbinu hizo ni matumizi ya nafsi ya kwanza umoja na wingi, tafsida, misemo, vitambulisho hadhi, takriri, ufutuhi, masimulizi ya hadithi na kuchanganya msimbo. Pamoja na mambo mengine, mbinu za kibalagha hutumika kulainisha lugha katika kufikisha ujumbe wa uwajibikaji, kuonesha mshikamano na kutoa matumaini. Aidha, mbinu za kibalagha hutumika kulinda utu wa watu, kusisitiza juu ya masuala mbalimbali, kuhimiza maendeleo na kuonesha falsafa ya kiuongozi kwa wananchi. Makala yanatoa mchango wa kimbinu katika uga wa isimujamii hususani katika lugha na siasa, kwa kudhihirisha namna vipengele anuwai vya kibalagha na jinsi vinavyoweza kutumika katika hotuba za viongozi wa kisiasa na vikaleta taathira njema kwa jamii.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.4

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-06-30

Issue

Section

Articles