Athari ya Mwachano Unaotokana na Umilisi wa Kipragmatiki kwa Wanafunzi wa Kiswahili nchini Rwanda

Authors

  • Mukamana Helene Chuo Kikuu cha Rwanda
  • Bisamaza Emilien Chuo Kikuu cha Rwanda

Abstract

Makala haya yamechunguza athari ya mwachano unaotokana na umilisi wa kipragmatiki kwa wanafunzi wa Kiswahili nchini Rwanda. Ingawa wanafunzi wa Rwanda wanajifunza Kiswahili kuanzia mwaka wa kwanza wa shule za upili, wanakabiliwa na changamoto za kimawasiliano ikiwa ni pamoja na umilisi wa kipragmatiki. Changamoto hiyo inatokana na mizizi ya kiutamaduni na kijamii ambayo si sawa na ustadi wa kisarufi. Changamoto hizi zinatokana na mizizi ya kijamii na kiutamaduni ya kipragmatiki ambayo si sawa na ustadi wa kisarufi. Utafiti huu, uliotumia Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles na Bryne (1992), ulijikita katika kuchunguza ujumbe wa wanafunzi kwa walimu kupitia simu na hojaji. Matokeo yanaonyesha kuwa wanafunzi wa Rwanda hukiuka kanuni za kipragmatiki za Kiswahili kutokana na athari za lugha yao ya kwanza (L1). Changamoto hiyo inasababishwa na umilisi wa pragmatiki wa L1 unaowaathiri wanafunzi katika matumizi ya Kiswahili (L2). Makala yanapendekeza njia za kukabiliana na changamoto hizi ili kuboresha mawasiliano ya wanafunzi katika Kiswahili.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.5

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-06-30

Issue

Section

Articles