Mtagusano wa Uolezi na Uhusika katika Uwasilishaji wa Ujumbe katika Riwaya ya Kiswahili

Authors

  • Dinah Sungu Osango Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Mwenda Mbatiah Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Timammy Rayya Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Makala haya yanachanganua mtagusano wa uolezi na uhusika katika riwaya teule za Kiswahili ili kuonesha jinsi aina mbalimbali za uolezi zinavyoathiri ujenzi wa wahusika na kushawishi uibukaji wa ujumbe katika riwaya za Kiswahili. Uchanganuzi wa uolezi  ni muhimu katika kutuonesha jinsi waandishi wanavyowatumia wahusika ili kuangazia masuala ya jadi au masuala ibuka ya kisasa katika jamii kwa kutumia mitazamo mbalimbali; na kwa njia hiyo, kufanya uolezi na uhusika kuwa mkakati wa kuwasilisha ujumbe mahususi kwa wasomaji. Uchunguzi wa suala la uolezi katika riwaya za Kiswahili unatokana na tafiti zilizopo kudai kuwa, uolezi ni suala ambalo halijatiliwa maanani katika tafiti za kifasihi zinazoangazia usimulizi wa riwaya ya Kiswahili. Riwaya ambazo zimetumiwa katika uchanganuzi wa makala haya ni: Haini (S.A. Shafi, 2002), Makuadi wa Soko Huria (C.S.L. Chachage, 2005), Ndoto ya Almasi (K. Walibora, 2006), Nyuso za Mwanamke (S.A. Mohamed, 2010), Harufu ya Mapera (K.W. Wamitila, 2012) na Hujafa Hujaumbika (F.M. Kagwa, 2018). Kwa kuwa riwaya hizi zina mawanda mapana, tumedondoa tu baadhi ya mifano ambayo inadhihirisha uolezi na uhusika ili kupata data ambazo zimetupa picha kamili kuhusu riwaya ya Kiswahili. Madhumuni ya uchanganuzi huu ni kutambulisha aina mbalimbali za uolezi na uhusika na uamilifu wake katika uwasilishaji wa simulizi. Uchunguzi huu umeongozwa na Nadharia ya Naratolojia ambayo inatambua uolezi na uhusika kama vipengele muhimu katika uwasilishaji wa simulizi.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.7

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-06-30

Issue

Section

Articles