Uhakiki wa Kimwingilianomatini katika Fasihi ya Watoto
Mambo ya Msingi ya Kuzingatia
Abstract
Kazi za fasihi ya watoto kama zilivyo kazi nyingine za fasihi ya Kiswahili zina mwingiliano wa matini wa kiwango cha juu. Hii ina maana kwamba, Nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva, ambayo hutumika kuhakiki kazi za fasihi ya watu wazima, hutumika pia kuhakiki kazi za fasihi ya watoto. Kuna mambo ya msingi kadhaa ambayo mtumiaji wa nadharia hii anapaswa kuyazingatia. Hivyo, makala haya yanalenga kubaini mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kuhakiki kazi za fasihi kwa kutumia Nadharia ya Mwingilianomatini. Ili kufikia lengo hili, makala yanaielezea nadharia husika ambapo mawazo yake makuu yanabainishwa na ubora wake kufafanuliwa. Kisha, kazi teule za fasihi ya watoto zinahakikiwa kwa kutumia Nadharia ya Mwingilianomatini. Kazi za fasihi za watoto zilizohusishwa katika makala haya ni Sababu mimi ni Mwanamke, Kilio Chetu, Ngome ya Mianzi na Marimba ya Majaliwa. Mwisho, makala yanabainisha mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kuhakiki kazi za fasihi kwa kutumia nadharia hii. Matokeo yanaonesha kuwa mhakiki anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo; kwanza, Nadharia ya Mwingilianomatini ina mawanda mapana. Pili, kiwango cha maarifa aliyonayo mhakiki kuhusu matini chanzo kinaweza kuathiri ufanisi wa uhakiki wa kazi ya fasihi. Tatu, Nadharia ya Mwingilianomatini ina njia bainifu anuai. Nne, Nadharia ya Mwingilianomatini kuhusisha matini zisizo za kifasihi.
DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.8