Uchambuzi wa Mitindo ya Kiepisto katika Riwaya za Kiswahili

Aina na Matumizi ya Lugha

Authors

  • Yusta Violet Mganga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Leonard Flavian Ilomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Fasihi inapitia mabadiliko na kupata maendeleo katika matumizi ya mitindo ya uandishi wa kazi za fasihi. Baadhi ya mitindo hii inajulikana kama mitindo ya kiepisto. Vinogradu na Skuortson (2014) wameeleza kuwa miongoni mwa mitindo ya kiepisto inayotokana na mawasiliano ya kielektroniki ni kama arafa, baruapepe, blogu, wakati mawasiliano kila siku ndani ya jamii ni kama vile barua na shajara. Mitindo hii imezoeleka kukidhi mawasiliano katika miktadha mbalimbali (Vinogradu na Skuortson, 2014). Kumekuwa na matumizi ya mitindo ya kiepisto katika kazi za fasihi. Mmojawapo wa wataalamu waliojadili mitindo ya kiepisto katika fasihi ni Mutembei (2016) aliyechunguza dhima ya mitindo ya kiepisto katika fasihi ya Kiingereza na Kiswahili, na kubaini matumizi ya mtindo wa kiepisto wa barua ingawa mitindo ya kiepisto ni mingi. Kutokana kutokuwa na maelezo ya kutosha ya kiutafiti kuhusu aina za mitindo ya kiepisto, makala haya yamechunguza mitindo ya kiepisto katika fasihi ya Kiswahili ili kubaini aina zake, na vipengele vya matumizi ya lugha katika mitindo hiyo. Data za mjadala huu zilipatikana maktabani kupitia usomaji makini. Nadharia ya Usemezano ya Bahktin (1980) na Nadharia ya Mtindo ya Leech (1969) zimetumika. Makala haya yalibaini mitindo ya kiepisto iliyotokana na mawasiliano ya kielektroniki kama: arafa, na baruapepe. Vilevile, mawasiliano yaliyotokana na nyaraka za mawasiliano ya kawaida kama: barua na shajara. Pia, makala haya yalibaini vipengele mbalimbali vya matumizi ya lugha vilijitokeza kama tashibiha, tasfida, majazi, taashira, methali, misemo na nahau kudhihirisha sanaa iliyomo katika mitindo ya kiepisto.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.10  

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-06-30

Issue

Section

Articles