Makosa ya Kiuandishi katika Kamusi za Kiswahili na Athari zake kwa Watumiaji

Authors

  • Jacob Haule Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa
  • Titus Mpemba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Lugha huenea na kuimarika kupitia kuandaa maandishi ya kusomwa na watu wengi duniani na ujumbe wa kimaandishi humfikia vizuri msomaji iwapo utaandikwa vizuri. Mbali na kufikisha ujumbe, uandishi mzuri pia huvuta makini ya msomaji ilhali uandishi mbaya humkanganya na kumchusha. Kwa kuwa kamusi hukusudiwa kuwa miongozo ya usanifu na ufasaha wa lugha husika, inatarajiwa kuwa zinaepuka makosa ya kiuandishi. Kwa kutumia Nadharia ya Urafiki wa Kamusi kwa Mtumiaji, makala haya yanahakiki kiwango cha uzingativu wa kaida ya uandishi mzuri katika kamusi za Kiswahili, yakilenga Kamusi Kuu ya Kiswahili (KKK), Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) na Kamusi la Kiswahili Fasaha (KKF). Ili kulifikia lengo hili, waandishi walijihususisha na kubainisha makosa ya kiuandishi tu na kujadili athari zake kwa wasomaji. Data zilikusanywa kupitia uchambuzi matini. Matokeo yanaonesha kuwa kamusi madhukura zina makosa ya udondoshaji na uchopekaji, matumizi muhali ya njeo, uradidi, unafasishaji usio sahihi, na upatanishi potofu wa kisarufi, ambayo ama huwakosesha watumia kamusi maana sahihi au huwachusha. Kutokana na matokeo haya, waandaaji na wachapishaji wa kamusi wanashauriwa kuweka jitihada za kuyaepuka makosa ya aina hii. Hili litahakikisha kuwa ujumbe wa kamusi unawafikia watumiaji kama ulivyokusudiwa na kuwaepushia athari zilizotajwa.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t1.3

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-06-30

Issue

Section

Articles