Uchanganuzi wa Kirai Kihusishi cha Kiswahili

Authors

  • Tumaini Mahendeka Taasisi ya Elimu Tanzania
  • Luinasia E. Kombe Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam

Abstract

Makala haya yanajadili muundo wa kirai kihusishi cha Kiswahili kwa kutumia mkabala wa sarufi miundo virai. Yanatambua kategoria tano za virai katika Kiswahili: virai nomino, virai kitenzi, virai kivumishi, virai kielezi, na virai kihusishi. Wataalamu wa sarufi ya Kiswahili wamekuwa wakitumia mkabala huu kuelezea muundo wa kirai kihusishi, lakini wanatofautiana kuhusu vijenzi vinavyohusishwa, jambo linalosababisha ukosefu wa urari katika uchanganuzi. Lengo la makala haya ni kubainisha muundo wa kirai kihusishi cha Kiswahili, kueleza sifa zake za kimuundo, na kufafanua sababu za kiisimu zinazowafanya wataalamu kutofautiana kuhusu uchanganuzi wa vijenzi vya kirai kihusishi licha ya kutumia mkabala mmoja wa sarufi miundo virai. Data zilichambuliwa kwa mbinu ya uchambuzi wa matini na mbinu ya uchambuzi wa maudhui. Matokeo yanaonesha kuwa kirai kihusishi kinaundwa na kihusishi kama neno kuu na kirai nomino au kishazi tegemezi kama vijalizo vyake. Neno kuu la kirai hutawala vijalizo vyake na halisimami peke yake. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa tofauti za kiisimu zinazofanya wataalamu watofautiane kuhusu uchanganuzi wa vijenzi za kirai kihusishi zinatokana na athari za tafsiri kutoka Kiingereza na kutokuzingatia kanuni za miundo virai.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t2.1

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-12-30

Issue

Section

Articles