Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Abstract
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawasiliano rasmi, hasa ikilinganishwa na Kiingereza. Lengo la utafiti lilikuwa kubainisha mikakati ambayo Kiswahili kinatumia kukua na kufanikisha mawasiliano rasmi. Data ilikusanywa kutoka kwa maandishi mbalimbali na Kamusi Pevu ya Kiswahili (2016). Utafiti huu uliozaa makala haya ulionesha kwamba Kiswahili kinatumia mikakati ya urekebu wa kifonolojia na kisemantiki kupata msamiati na istilahi za kufanikisha mawasiliano. Utafiti unapendekeza kuundwa kwa chombo cha kitaifa kusimamia maendeleo ya msamiati wa Kiswahili na kupendekeza Kiswahili kiweze kutumika katika mawanda yote, yakiwemo rasmi, ili kiweze kufanikisha majukumu yake mapya. Aidha, makala haya yanapendekeza kuwa Kiswahili kinastahili kutumiwa katika mawanda yote ili kiweze kurekebu na kuyafanikisha majukumu yake mapya ya kimawasiliano kama lugha rasmi nchini Kenya.
DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t2.2