Uhusiano wa Wapemba na Wamakonde
Hoja za Kihistoria
Abstract
Makala haya yanahusu uhusiano wa Wapemba na Wamakonde kwa kuegemea katika hoja za kihistoria. Data za utafiti uliozaa makala haya zimekusanywa kwa njia ya usaili, hojaji na ushuhudiaji katika maeneo ya Kisiwa cha Pemba na katika mkoa wa Mtwara. Uchambuzi wa data umeongozwa na nadharia mbili ambazo ni Nadharia ya Mwachano na Makutano ya lugha za Kibantu na Nadharia ya Isimu Historia Linganishi. Data za makala haya zimechambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli Matokeo ya utafiti uliozaa makala haya yanaonesha kuwa kuna uhusiano wa karibu wa kihistoria baina ya Wapemba na Wamakonde unaotokana na sababu mbalimbali kama vile kuhamahama, kukimbia vita, kuoana na suala la shughuli za uchumi na biashara.
DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t2.4Downloads
Download data is not yet available.