Miundo ya Vishiriki vya Kitenzi Isiyofuata Udarajia wa Dhima za Kisemantiki katika Sentensi za Kiswahili

Authors

  • Oliva Mang'ita Chuo Kikuu cha Dodoma
  • Fabiola Hassan Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Makala haya yanahusu miundo ya vishiriki vya kitenzi isiyofuata Udarajia wa Dhima za Kisemantiki katika sentensi za Kiswahili. Msingi wake ni ukiukwaji wa Udarajia wa Dhima za Kisemantiki katika miundo ya vishiriki vya kitenzi katika sentensi za Kiswahili. Kwa mujibu wa udarajia, dhima za kisemantiki zipo katika mpangilio kuanzia nafasi ya juu kuelekea nafasi ya chini kulingana na uwezo wa dhima husika kuwa kiima cha sentensi. Kwa mujibu wa mpangilio huo, dhima iliyopo katika nafasi ya juu (kushoto) inapaswa kuwa kiima kuliko dhima iliyopo katika nafasi ya chini kuelekea kulia. Hata hivyo, ipo miundo inayokiuka utaratibu huu. Katika miundo hiyo, kishiriki chenye dhima ya kisemantiki iliyopo katika nafasi ya chini huhusishwa na kiima ilhali kuna vishiriki vyenye hadhi ya kuwa kiima. Makala haya yanafafanua miundo inayokiuka udarajia katika sentensi za Kiswahili. Data zilipatikana kwa njia ya uchambuzi matini, hojaji na upimaji wa usahihi wa kisarufi. Uchanganuzi wa data umetumia misingi ya Nadharia ya Sarufi Leksia Amilifu ya Bresnan na Kaplan (1970). Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, katika Kiswahili, kuna miundo isiyofuata udarajia. Kutokana na matokeo haya, makala yanahitimisha kwamba ipo miundo isiyofuata udarajia. Katika miundo hiyo, kuna upandishaji hadhi wa dhima iliyopo katika nafasi ya chini katika udarajia.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t2.5

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-12-30

Issue

Section

Articles