Uakisikaji wa Udongo kama Suala la Kiikolojia katika Ushairi wa Kiswahili

Mfano kutoka Ushairi wa Mohammed na Mberia

Authors

  • Mugwe Mwaniki Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Omboga Zaja Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Rayya Timammy Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Uakisikaji wa udongo katika ushairi wa Kiswahili umewahi kujitokeza kama motifu tata ya kimaudhui yenye wingi-maana itumiwayo kuzungumzia masuala ya kitamaduni. Aidha, hutumiwa kuzungumzia masuala ya kiroho na utathmini wa thamani za kiikolojia zinazohusiana na ufahamu wa mazingira na ikolojia. Uakisikaji huo, katika ushairi, unapochanganuliwa kwa kuegemezwa katika mihimili ya Nadharia ya Uhakiki wa Kiikolojia, unajitokeza kama kioo cha kuangazia mahusiano fungamani yaliyopo kati ya binadamu na mazingira asili. Makala haya yanachunguza uakisikaji wa udongo kama suala la kiikolojia katika ushairi wa Mohamed na Mberia katika diwani za Kina cha Maisha (Mohamed, 1984), Jicho la Ndani (Mohamed, 2002), Msimu wa Tisa (Mberia, 2007) na Rangi ya Anga (Mberia, 2014). Tungo hizi zinatumiwa kama sampuli lengwa. Uchanganuzi wa data umewasilishwa kwa njia ya maelezo yanayojumuisha nukuu za beti pamoja na ufafanuzi wake. Mjadala umekitwa katika Nadharia ya Uhakiki wa Kiikolojia iliyoasisiwa na Glotfelty (1996). Nadharia hii inazungumzia mwingiliano uliopo kati ya mazingira ya asili na binadamu katika tungo za fasihi. Mwingiliano huu katika mashairi haya unawasilishwa kupitia visa, mienendo na taratibu za matumizi ya udongo yaliyo na athari hasi na chanya kwa mduara wa ikolojia.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t2.6

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-12-30

Issue

Section

Articles