Mla

Kiunzi cha Uzingatizi wa Maadili ya Waswahili katika Methali Teule za Kiswahili

Authors

  • Martina Duwe Chuo Kikuu Mzumbe

Abstract

Thamani ya Mla hubainika kupitia mahangaiko ya kusaka mlo utakaomfaa yeye na jamii yake kwa jumla. Katika mahangaiko hayo, Mla huweza kutenda kinyume na maadili yanayopaswa kuzingatiwa na jamii yake. Matendo hayo huweza kumwathiri yeye au/na jamii inayomzunguka. Kwa kuzingatia hilo, methali za Kiswahili zimesukwa kwa ufundi unaobainisha namna Mla anavyoweza kuzingatia maadili kulingana na maisha halisi ya Waswahili. Hata hivyo, haiko bayana ni kwa namna gani methali zenye kufungamanishwa na neno ‘mla’ zinavyobeba umahususi wa uzingatizi wa maadili kwa Mla. Kwa msingi huo, makala haya yanafafanua namna methali zenye kumrejelea Mla zinavyobeba na kudokeza maarifa mbalimbali ya kimaadili kulingana na kaida za jamii.  Ili kufanikisha hilo, ilitumika mbinu ya uchambuzi matini ambapo methali zenye kuhusishwa na neno ‘mla’ zinazotumiwa na Waswahili zilisaidia katika kupata data za matokeo haya. Vilevile, katika makala haya, imetumika Nadharia ya Uhalisia kama mwegamo mkuu katika kuchunguza, kuchanganua na kuwasilisha data husika. Matokeo yanaonesha kuwa dhana ya mla katika methali za Waswahili haijatumika kimakosa, bali imelenga kusisitiza na kuhifadhi maarifa mbalimbali ya kimaadili yanayotosheleza utamaduni wao. Kwa hiyo, makala haya yanajadili kwa kina vipengele vya maadili vinavyosisitizwa kwa Mla kupitia methali teule za Kiswahili. Vipengele hivyo vya kimaadili ni: kuthamini na kuheshimu udugu, kutambua tabia za watu, kuthamini wakati wa sasa, kuwajibika na kujituma katika kufanya kazi, kutambua athari za kupokea hisani na kutambua athari za wema na ubaya.

DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na43t2.7

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2024-12-30

Issue

Section

Articles