MWELEKEO MSETO KATIKA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KISWAHILI

Authors

  • Opunde Shadrack CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA CHA MASINDE MULIRO- KAKAMEGA KENYA

Abstract

Mwelekeo mseto katika ufundishaji wa lugha si dhana mpya katika mitaala ya elimu kwa sababu masomo ya sarufi na fasihi ya Kingereza yamekuwa yakisetwa, haswa katika Silabasi ya shule za upili. Ufundishaji lugha umepitia awamu na hatua mbalimbali kutegemea mabadiliko na mahitaji ya kijamii ulimwenguni. Dhana ya usetaji katika ufundishaji wa lugha ina misingi yake katika elimu kama mfumo mzima. Silabasi ya K.I.E 2002 ilipendekeza ufundishaji wa lugha uegemee katika mwelekeo mseto ambao unampa mwanafunzi ukati na ushiriki mkubwa wakati wa ufundishaji.

Hata hivyo utekelezwaji wa mwelekeo mseto katika ufundishaji wa Kiswahili bado ni changamano. Baadhi ya maswali ambayo walimu wameshindwa kuyaweka bayana ni kama vile; Nini maana ya dhana ya mwelekeo mseto? Ni Maudhui gani ambayo yanapaswa kusetwa? Yanafaa kusetwa kwa wakati gani na kwa kutumia njia, mbinu na vifaa gani?Makala hii inalenga kujibu baadhi ya haya maswali ili kudhihirisha namna mwelekeo mseto unaweza kutumiwa katika ufundishaji wa Kiswahili hasa namna matini ya fasihi yanaweza kutumiwa katika kutoa muktadha wa ufafanuzi wa vipengele vya sarufi.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2017-08-21

Issue

Section

Articles