NGELI ZA NOMINO ZA KI-MICHEWENI
Abstract
Makala hii inachunguza na kuainisha ngeli za nomino katika Ki-Micheweni. Data iliyotumika katika makala hii imekusanywa kutoka uwandani kuanzia mwezi Januari hadi Machi, 2015. Uchambuzi na uwasilishaji wa data iliyotumika katika makala hii umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Asilia ya Dressler (1985). Nadharia hii hubainisha viambishi awali vya nomino na dhima zake kisemantiki. Matokeo ya uchunguzi huu yanabainisha kuwa Ki-Micheweni kina ngeli za nomino 18. Kwa kutumia mkabala wa viambishi awali vya nomino tumeweza kuainisha kwa kutenga viambishi vya nomino vya umoja na wingi katika ngeli tofauti katika uainishaji wa msingi. Hali kadhalika, katika uainishaji mdogo wa ngeli za nomino tumeona kuwa ngeli zenye mtawanyiko ni zile zinazohusu wanyama, sehemu za mwili na vitu visivyo hisivu. Aidha, tumebaini kuwa dhima za kisemantiki kama vile, ukubwa, tabia mbaya na dhihaka zipo katika ngeli ya 5/6 na hali ya udogo, ubaya, uzuri zipo katika ngeli 7/8. Hapa tumebaini tofauti kati ya Ki-Micheweni na lugha nyingine za Kibantu. Kwa sababu Kahigi (2005) anaeleza kuwa dhima ya udogoshaji katika lugha za Kibantu zinapatikana katika ngeli ya 12/13 pekee.