Mtindo na Maudhui katika Nyimbo za Kisiasa za Msanii John De ' Mathew nchini Kenya
Abstract
Makala hii inafafanua mitindo inayotumiwa na mwanamuziki John De ' Mathew katika kuwasilisha ujumbe wa kisiasa. Nyimbo zimetumika katika miktadha na nyakati mbalimbali kufafanua masuala anuwai yanayomwathiri binadamu. Pia, hutumika kuhamasisha, kutia moyo, kuchokoza na hata kuchochea watu kutenda matendo mbalimbali. Utunzi wa nyimbo, kama ilivyo katika tanzu zingine za fasihi, huhusisha matumizi ya mitindo changamano ili kuwasilisha ujumbe unaodhamiriwa. Makala hii inalenga kutambulisha, kuainisha na kuchanganua vipengele vya kimtindo vinavyotumiwa na mwanamuziki John De ' Mathew anapotunga nyimbo zenye maudhui ya kisiasa nchini Kenya. Aidha makala pia inaangazia baadhi ya maudhui ya kisiasa yanayopatikana katika nyimbo hizo. Nyimbo zake tano zilichaguliwa kimakusudi na kuchanganuliwa. Matokeo yanadhihirisha kwamba msanii huyu ametumia mitindo mbalimbali katika kuwasilisha ujumbe wa kisiasa katika nyimbo zake.