Maana katika Majina ya Wabena nchini Tanzania
Abstract
Jina, kulingana na Plato, ni aina ya maneno na ni njia pekee ya kurejelea dhana au kitu. Maana ilihusishwa na jina na ujinaishaji (Resani, 2015). Kutokana na umuhimu wa jina, binadamu wamepewa na kupeana majina kama kitambulisho cha kuwatambulisha miongoni mwa jamii husika. Kila jamiilugha ina majina ambayo huitambulisha zaidi, lakini ukweli unabaki kuwa kila jina apewalo mtu lina maana na athari kwa mhusika. Katika makala hii tumejadili maana ya majina wapewayo watu wa jamii ya Wabena. Kabla ya ufafanuzi wa majina hayo imeelezwa historia ya Wabena ikionyesha shughuli zao za kiuchumi, eneo lao la kijiografia wanalopatikana na majirani wanaowazunguka. Makala kwa undani inaeleza chanzo cha majina, maana na athari ya majina kwa mwenye jina katika jamii ya Wabena mkoani Njombe nchini Tanzania.