Tafsiri za Fasihi ya Kiswahili na Mchakato wa Utandawazi

Clara Momanyi

Abstract


Katika muktadha wa ubadilishanaji wa maarifa, ujuzi na sayansi, utandawazi si dhana ngeni. Hii ni kwa sababu ubadilishanaji huu miongoni mwa nchi mbalimbali uliwezeshwa na mchakato wa utandawazi mkongwe uliokita mizizi hususan katika karne za 16 hadi 19. Tamaduni nyingi ulimwenguni zimeweza kupiga hatua za kimaendeleo kutokana na ubadilishanaji wa habari na maarifa kwa njia ya tafsiri. Sanaa za uandishi miongoni mwa jamii mbalimbali za ulimwengu zimepokezwa kwa muda mrefu kupitia tafsiri. Mchepuo wa lugha na taaluma za tafsiri vilichangia na vinaendelea kuchangia kasi ya utandawazi huo na hivyo, kuzijenga na kuziimarisha tafsiri za fasihi mbalimbali ulimwenguni. Kutokana na uhalisi huu basi, makala yanalidurusu suala la tafsiri za kifasihi hususan katika muktadha huu wa utandawazi. Aidha, yanajadili umuhimu wa tafsiri za matini za fasihi ya Kiswahili katika mawanda ya utandawazi kwa kuzingatia faida zake katika kueneza utamaduni, falsafa na maadili yetu.


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.