Tafsiri katika Fasihi ya Watoto: Mbinu na Mikakati

Authors

  • Pamela M.Y Ngugi

Abstract

Makala[1] haya yanahusu masuala ya fasihi ya watoto, tafsiri na usilimishwaji. Kutafsiri fasihi ya watoto ni jambo lisilo rahisi. Mbali na kuwa kazi ya tafsiri inabadilisha matini ili kuweza kupata faida fulani, ipo mikakati chungu nzima inayohitaji kuzingatiwa katika kazi ya kutafsiri fasihi ya watoto. Muhimu kuzingatia ni kwamba walengwa wa tafsiri hii wanazo tajriba finyu mno kuhusiana na lugha, ukuaji na ujuzi wa mambo ya kijamii. Hivyo basi wafasiri hukumbana na matatizo ya kuzitafsiri na kuzisilimisha kazi hizi ili ziweze kufikia kiwango cha uelewa cha walengwa. Kama anavyodai Thomson-Wolgemuth (1998), "Zipo hatari nyingi fiche katika harakati ya kutafsiri fasihi ya watoto kwa sababu ni rahisi kwa wafasiri kusahau kutilia maanani shauku za mtoto". Lengo la makala haya ni kujaribu kubainisha mbinu na mikakati inayotumika katika kutafsiri fasihi ya watoto.


 

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2017-08-11

Issue

Section

Articles