Tungo za Kinahau Zinazotoa Taarifa ya Mpira wa Miguu katika Magazeti ya Kiswahili

Authors

  • Sabra Ahmed

Abstract

Makala haya yanachambua tungo za kinahau zinazotoa taarifa ya mpira wa miguu katika magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania. Kazi hii inajikita kuchambua maana mbalimbali za kimazingira zinazotokana na tungo za kinahau zinazotumiwa na waandishi wa magazeti katika kutoa taarifa za mpira wa miguu. Makala pia yanabanisha vigezo ambavyo waandishi hutumia katika kuchagua tungo za kinahau kutoa taarifa zao. Halikadhalika, makala yanabainisha wazi sababu zinazopelekea waandishi wa ripoti za mpira wa miguu kutumia tungo hizo za kinahau. Mbali na hayo, data za makala haya zimepatikana kwa njia ya kusoma magazeti ya michezo pamoja na kusaili waandishi 40 wa magazeti ya michezo. Magazeti yaliyotumiwa na makala haya ni Bingwa, Lete Raha, Spoti Starehe, Burudani, Mwana Spoti na Dimba.   Mwandishi ameteua magazeti haya ili kuweza kupata data halisi kuhusiana na tungo za kinahau zinazotumiwa na waandishi kutoa taarifa za mpira wa miguu. Pia, mwandishi wa makala haya ameteua taarifa za   mpira wa miguu kwa sababu waandishi wa taarifa hizi hutumia kwa kiasi kikubwa tungo za kinahau ili kuvuta wasomaji wao pamoja na kuuza magazeti yao. Utafiti huu ulitumia data zilizokusanywa mwaka 2009. Msingi unaoongoza makala haya ni kuwa lugha hupata maana kulingana na mazingira inamotumika.

 

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2017-08-11

Issue

Section

Articles