Kutoka Futuhi hadi Ufutuhi: Chimbuko, Maendeleo na Nadharia zake
Abstract
Makala haya yanaijadili dhana ya ufutuhi ambayo bado haijazoeleka kimatumizi katika fasihi ya Kiswahili. Makala yanajikita katika kujadili jinsi ufutuhi ulivyochimbuka kutoka katika dhana-mama ya futuhi, na kupata mwelekeo mpya wa kimatumizi. Ufafanuzi unaanzia kwenye mgongano wa kiistilahi kuhusu dhana kadhaa zinazotumiwa kumaanisha vipengele na matokeo ya ufutuhi. Kisha, umefuatia ufafanuzi unaoangazia maendeleo ya dhana ya ufutuhi kutokea kwenye fikra za futuhi; mwisho kuna maelezo ya kinadharia kuhusu utokeaji wake. Nadharia zilizojadiliwa ni tatu; nazo ni Nadharia ya Mkwezo, Nadharia ya Msigano, na Nadharia ya Burudiko. Mjadala umefanywa kwa shabaha ya kuijengea uhalali dhana hii mpya na jumuifu ili kupunguza matatizo ya mwingiliano na uradidi unaojidhihirisha katika kuzitumia dhana kama vile kejeli, dhihaka, tashtiti, utani, ucheshi, kicheko, na furaha ambazo zinaendana na ufutuhi.