Athari ya Muktadha katika Utunzi wa Kazi za Mathias Mnyampala

Authors

  • Anna N. Kyamba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Abstract

Makala hii inakusudia kuchunguza athari ya muktadha katika utunzi wa kazi za Mathias Mnyampala. Hii inatokana na ukweli kwamba hakuna kazi ya fasihi inayoibuka katika ombwe. Kwa kawaida kazi mbalimbali hutungwa kwa kuzingatia miktadha anuwai kama vile wa kijamii, kisiasa, kiuchumi na kijiografia. Wapo watunzi wengi wa fasihi ya Kiswahili waliotunga kazi za fasihi katika nyakati tofauti, lakini miktadha ya utunzi wa kazi zao haijajulikana kikamilifu. Mmojawapo wa watunzi hao ni Mathias Mnyampala. Kwa ujumla, katika uwanja wa fasihi mtaalamu huyu amesahaulika katika uhakiki na uchambuzi wa kazi zake (Madumulla, 2011; Kyamba, 2018). Kadhalika katika uhakiki wa kazi za mtaalamu huyu muktadha wa utunzi umegusiwa tu na baadhi ya watafiti pasipo kufanya uchambuzi. Mulokozi (2017) anaeleza kuwa ni muhimu kuzingatia muktadha wa mwandishi katika uhakiki wa kazi ya kisanaa ili ieleweke kikamilifu. Kutokana na umuhimu wa suala hilo, makala hii inakusudia kuchunguza athari ya muktadha katika utunzi wa kazi za Mathias Mnyampala. Makala hii imetumia vitabu vinne vya ushairi. Aidha, makala imeongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini ya Julia Kristeva ya mwaka 1960 inayosema kuwa hakuna kazi ya inayoibuka katika ombwe. Kwa kutumia nadharia hii, tumebaini kuwa muktadha wa utunzi wa kazi za Mnyampala unaingiliana, unakamilishana na unategemeana na matini nyingine tangulizi.

 

http://doi.org/10.56279/jk.v85i1.4

Author Biography

Anna N. Kyamba, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Mhadhiri

Published

2023-03-17

Issue

Section

Articles