CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI FASIHI YA WATOTO NCHINI TANZANIA

Authors

  • L H Bakize

Abstract

Fasihi ya watoto ikilinganishwa na fasihi ya watu wazima bado ni changa katika Afrika Mshariki, Afrika na duniani kwa ujumla. Mathalani, katika Bara la Afrika, fasihi hii inayowalenga na kuwahusisha watoto kwa upekee wao ilishamiri na kushika mizizi katika karne ya kumi na nane na kumi na tisa (Traore, 2010 na Bakize, 2014). Nchini Tanzania kwa mfano, fasihi hii imeota mizizi na kuchipuka zaidi miaka ya 1990 hasa baada ya kuzinduliwa kwa Mradi wa Vitabu vya Watoto mwaka 1991. Kuanzia hapo mradi huo umeisogeza mbele fasihi ya watoto kwa kutoa semina ya uandishi kwa waandishi chipukizi, kuwafadhili na kufikisha kazi zao katika shule chache za msingi zilizoteuliwa kuwa sehemu ya mradi. Mpaka sasa mradi huo unakadiriwa kuwa umewezesha uchapishaji wa vitabu zaidi ya 350. Pamoja na dalili hizo nzuri za kupiga hatua kwa fasihi ya watoto nchini Tanzania, bado changamoto zinazoikabili fasihi hiyo ni nyingi. Makala haya yanabainisha changamoto hizo na kutoa mapendekezo ya kukabiliana nazo.

 

Downloads

Published

2017-08-11

Issue

Section

Articles