RUWAZA ZA SHUJAA NA UIBUAJI WA DHAMIRA: MIFANO KUTOKA UTENDI WA GILGAMESH

Sosoo Felix Kwame

Abstract


 

Hagin (2007)anafafanua kwamba, utendiniushairimrefuwamasimulizijuuyamatendoya utukufu ya shujaa ambaye si Mungu bali ni binadamu. Emmanuel (2013:33) anatuambia kwamba, utendiniutanzuwadunianzimana kwamba, tendi zotezinazojulikana huwa na matukio yanayofanana na yanaweza kuwa ya kihistoria na visakale au visasili. Kwa hali hiyo, tunashawishika kusema kuwa utendi wa Gilgameshunahusu matukio ya kishujaa ambayo yanaweza kuwa ya kweli, ya uongo au ya kubuni, yenye kutoa mafunzo fulani katika jamii za kilimwengu. Kwa kuzingatia fasili hizo hapo juu, makala haya yanakusudia kuuchambua utendi wa Gilgamesh, ili kuchunguza namna ruwaza ya shujaa wa utendi inavyoweza kuibua dhamira kwa lengo la kuifunza jamii iliyotajwa hapo juu. Makala yanaanza kwa utangulizi wa jumla na yanaelezea jinsi utendi wa Gilgamesh ulivyoibuka katika fasihi ya Kiswahili. Kadhalika, makala yanaongozwa na mkabala wa kinadharia katika kuchambua ushujaa unavyoibua dhamira kwa kupitia vipengele teule vya kiuchambuzi.


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.