Mchango wa `Kiriku` Katika Makuzi ya Fasihi ya Watoto

Deborah Nanyama Amukowa

Abstract


Fasihi ya kiafrika imekua na kujipambanua miongoni mwa waatalam wa fasihi ya Kiswahili. Kuibuka kwa sanaa ya maonyesho kupitia vibonzo ni mwamko ambao umo miongoni mwa wataalam wa fasihi ya Kiswahili. Hii ni njia mojawapo ya kuonyesha maendeleo katika fasihi ya watoto. Ni jambo jema na linaloafikiana na matukio yanayohusu mwamko wa fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Umuhimu wa sanaa ya vibonzo katika kazi za fasihi ni kwamba, inapambanua taaluma ya fasihi ya watoto. Katika enzi hii ya utandawazi, vibonzo husimulia matukio, huelimisha, huonyesha, huonya na kutoa taarifa kuhusu maendeleo kwa njia ya kisanaa kupitia ubunifu hasa baada ya uvumbuzi wa teknolojia ya kutumia vyombo vya kielektroniki. Huu ni mwamko mpya katika fasihi ya Kiswahili unaobainisha kuwa fasihi hii imo katika kipindi cha mabadiliko na hasa katika fasihi ya watoto ambayo ilianza kupitia hadithi simulizi na nyimbo. Hii ni fasihi maalum inayotungwa kwa ajili ya watoto na huweza kuwa hadithi, ushairi au drama. Huwa na sifa maalumu ambazo pia hubainika katika masimulizi ya vibonzo. Mtunzi hufanikiwa kuvuta makini ya watoto anapozua njia mpya zenye mvuto. Ingawa matumizi ya wahusika wanyama huwavutia sana watoto, mvuto huo pia unawezabainika kupitia matumizi ya vibonzo. Hali hizi hubainisha tamaduni halisi za jamii husika. Hivyo basi, ni njia mojawapo ya kufufua tamaduni na wakati huo huo kujifunza kutokana na tamaduni za kigeni.

 


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.