Maadili ya Kisiasa Katika Riwaya za Kiswahili: Kufa Kuzikana na Babu Alipofufuka

Justus Kyalo Muusya, Kitula King’ei King’ei

Abstract


Uongozi wa jamii huathiriwa na maadili ya viongozi wake. Viongozi wanapozingatia maadili uongozi wao huwa mwema. Wakikosa kuzingatia maadili uongozi wao huwa potovu. Makala haya yanadhamiria kuchunguza namna ambavyo waandishi wa riwaya wameweza kusawiri suala hili. Riwaya zilizotumiwa katika makala haya ni Kufa Kuzikana (Walibora 2003) na Babu Alipofufuka (Mohamed 2001). Tathmini hii imeongozwa na nadharia ya daindamano. Daindamano ni mtazamo unaochukulia kwamba viongozi hutarajiwa kuhakikisha kwamba vitendo vyao ni vizuri na vinavyokubalika katika jamii. Matendo yao yanapaswa kuwa na manufaa kwa wananchi wengi. Hata hivyo, mtazamo huu huwapa viongozi nafasi ya kutekeleza baadhi ya maazimio ambayo japo yanaweza kuwaumiza wachache, huleta manufaa makubwa kwa watu wengi. Riwaya hizi zimeteuliwa kwa makala haya kwa vile waandishi wake wana uzoefu mkubwa katika uandishi na hasa wa riwaya. Kazi zao za kifasihi zimepata wahakiki wengi katika Afrika Mashariki na kwingineko. Wahakiki wa fasihi wanakubaliana kwamba Mohamed na Walibora wamekuwa wakisawiri jamii kimaadili na kisiasa kwa jicho pevu. Lengo la makala haya ni kujaribu kuonyesha jinsi riwaya za Kufa Kuzikana na Babu Alipofufuka zinavyowiana au kutofautiana katika kusawiri maadili ya wanasiasa katika jamii. Je, kuna mfungamano kati ya maadili ya kisiasa na uongozi wa jamii? Na je, jambo hili linadhihirika vipi katika riwaya ya Kiswahili ya kisasa?


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.