Nafasi ya Lugha katika Kukabiliana na Changamoto za Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa Afrika

Prisca Jebet Kiprotich

Abstract


Lugha ni kipawa cha kipekee kwa mwanadamu. Ni mali ya jamii ambayo kila mwanajamii huifurahia. Ni chombo muhimu cha mawasiliano katika jamii. Wataalamu wa lugha wanakubaliana kwamba lugha ni njia yoyote ya kuwezesha viumbe kuwasiliana, kuelewana na kupashana habari. Ni njia kuu na ya kimsingi katika mawasiliano ya binadamu. Kupitia lugha, binadamu anaweza kutambua utamaduni wa jamii, kwani lugha ni usajili wa utamaduni fulani.Jinsi ambavyo zipo jamii nyingi za tamaduni mbalimbali duniani, vivyo hivyo kuna lugha mbalimbali zilizoundwa ili kukidhi haja ya mawasiliano ya tamaduni hizi. Binadamu huweza kuendelea zaidi iwapo ana mbinu ya mawasiliano inayoeleweka na watu wengi. Ni kupitia kwa lugha ambapo binadamu ataweza kukabiliana na changamoto anazokumbana nazo katika shughuli za kila siku. Katika makala hii, tutachambua nafasi ya lugha katika kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Aidha, tutajadili changamoto mbalimbali zinazochangia katika kudidimisha lugha za kienyeji (za asili) Afrika ambazo ni pamoja na lugha za kienyeji kukosa kuhifadhiwa kimaandishi, mwongozo duni wa sera za lugha na udunishaji wa lugha za kienyeji miongoni mwa Waafrika wenyewe. Lugha za kienyeji zinahitaji kukuzwa na kuendelezwa kwa sababu ndizo zinazozungumzwa na asilimia kubwa ya jamii za Kiafrika. Hatimaye tutatoa mapendekezo kuhusu changamoto zinazodunisha lugha za kienyeji Afrika

Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.