Maudhui na Mawanda

Kioo cha Lugha ni jarida la kimataifa linalochapishwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI). Jarida linachapisha makala zinazohusu lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili na za lugha nyingine za Kiafrika. Vilevile, jarida linahamasisha mijadala na mapitio, hususani katika masuala ya sasa yanayohusiana na lugha na fasihi. Tungo fupi za masimulizi na ushairi zinakaribishwa pia. Jarida hili limekuwa likichapishwa mara moja kwa mwaka, lakini kuanzia mwaka 2021 lilianza kuchapishwa mara mbili kwa mwaka.

 

 

ISSN 0856-552 X (nakala ngumu) & ISSN 2546-2210 (mtandaoni)