Kiswahili

Kiswahili is an interdisciplinary international journal devoted to the study of Kiswahili language, linguistics and literature. Its main aim is to gather and disseminate under a single cover a wide variety of research and discussion of fundamental concern to all those scholars who have an interest in Kiswahili language, linguistics and literature.

 


HABARI ZA MKONDONI/ INDEXING AND ABSTRACTING

This journal can be accessed at the African Journals Online at the following link http://www.ajol.info/index.php/ksh/index, at the University of Dar es Salaam Journals online at the following link http://journals.udsm.ac.tz/index.php/kiswahili/index and also at the following link https://mft.ebscohost.com

KAMATI YA UHARIRI/EDITORIAL COMMITTEE

 

 

Prof. K.K. Kahigi  (Chief Editor)          

University of Dar es Salaam

Bw F.N. Joster  (Associate Editor)         

University of Dar es Salaam

Dkt. E.S. Mosha

University of Dar es Salaam

Dkt. S.S. Sewangi                      

National Kiswahili Council

Prof. Clara Momanyi     

Catholic University of Eastern Africa

Dkt. P.M.Y. Ngugi               

Kenyatta University

KAMATI YA USHAURI/ADVISORY COMMITTEE

Prof. D.J. Mkude

Chuo Kikuu Dar es Salaam

Prof. H. Batibo

Chuo Kikuu cha  Botswana

Prof. R. Mukama

Chuo Kikuu cha Makerere

Prof. F’ Topan

Chuo Kikuu cha London

Prof. K. King’ei

Chuo Kikuu  cha Kenyatta

Prof. E. Kezilahabi

Chuo Kikuu cha  Botswana

Prof. Doz. Dkt. Sc. K. Legère

Chuo Kikuu cha  Viena


ADA KWA MWAKA/ANNUAL SUBSCRIPTIONS

Afrika Mashariki/East Africa                                           Tshs. 5,000

Kwingineko/Elsewhere                                                       US$ 60.00 (kwa ndege/airmail)

MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA 

KISWAHILI ni jarida la kimataifa la taaluma ya Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu.

Jarida huchapishwa mara moja kwa mwaka. Tunapokea makala zilizoandikwa kwa Kiswahili na Kiingereza zikiwa zimeambatana na ikisiri fupi inayoeleweka. Makala zipigwe chapa kwenye karatasi za A4, mistari ikitengwa kwa kipimo cha nafasi mbili. Upande mmoja tu wa katarasi utumiwe.

Mwandishi awasilishe kwa Mhariri nakala tatu ngumu za muswada wake pamoja na nakala moja laini inayotangamana na Word 97-2003 au Word 2007.

Ukurasa wa kwanza wa makala uonyeshe jina la makala, jina kamili la mwandishi wa makala (ikiwa ni pamoja na wadhifa wake) na anwani yake.

Ukurasa wa pili uoneshe jina la makala na ufupisho wa makala kwa maneno yasiyozidi 300.

Unapotaja marejeo katika matini, taja jina la mwisho la mwandishi likifuatiwa, katika mabano, na mwaka wa chapisho hilo na kurasa zilizorejelewa, k.m. Mwanza (1985: 22). Kwenye orodha ya marejeo au bibliografia majina ya warejelewa yapangwe kialfabeti, ukianza na jina la mwisho la mwandishi na kufuatia na mwaka wa kuchapishwa katika mabano (k.m. Massamba, D.P.B. (1982)…).

Tanbihi zote ziwekewe namba na zitumike pale tu inapobidi. Maelezo ya tanbihi yatolewe kwenye ukurasa wa peke yake kufuatia mwisho wa makala, yaani kabla ya kuorodhesha marejeo.

Makala zitatathminiwa na angalau wasomaji wawili na zitarejeshwa kwa mwandishi pale tu ambapo gharama za usafirishaji zimelipwa. Baada ya makala kuchapishwa, waandishi wa makala hizo watapatiwa nakala moja ya Jarida lenye makala zao pamoja na malopoo kumi ya makala.

TANBIHI

Inapotokea kwamba kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu tukashindwa  kutoa juzuu lolote la jarida hili katika mfululizo wake wa kawaida, jitihada zitafanywa  kuhakikisha kwamba linatolewa Toleo Maalumu mapema iwezekanavyo  litakalozingatia makala zote zilizokuwa zimekusudiwa kutolewa katika jarida hilo ambalo lilikuwa limechelewa kutolewa.

INSTRUCTIONS TO CONTRIBUTORS 

KISWAHILI is an interdisciplinary international journal devoted to the study of Kiswahili Language, Linguistics and Literature. Its main aim is to gather and disseminate under a single cover a wide variety of research and discussion of fundamental concern to all those scholars who have an interest in Kiswahili Language, Linguistics and Literature.

The Journal comes out once a year. We accept papers and articles of scholarly standard written in Kiswahili and English, with clear abstracts. Manuscripts should be typed, double spaced on A4 size paper. Only one side of the page should be used.

Three copies of the manuscript should be sent to the editor with a soft copy compatible with Word 97-2003 and Word 2007.

The first page of each article should bear the title of the paper, and the full name (including title/position, academic affiliation, etc.) and address of the author.

The second page should bear the title of the paper and an abstract of not more than 300 words.

When mentioning references in the text, cite only the last name of the author followed (in brackets) by the date of publication and page(s), e.g. Mwanza (1985: 22). For all references/bibliography the names should be in alphabetical order, beginning with the last name of the author, followed in brackets, by year of publication (e.g. Massamba, D.P.B. (1982)…).

Notes should be numbered and used only for substantive information. These should be separated from the text, and should appear just before the bibliography.

Manuscripts will be sent to at least two reviewers and will only be returned if accompanied with a prepaid, self-addressed envelope. After publication, authors of full articles will receive a free copy of the journal and ten offprints of their articles.

NB:

We would like to inform our esteemed readers and authors of articles that in cases where, for reasons beyond our control, we fail to produce any journal issues at the appropriate time, efforts will be made to make sure that a Special Issue be produced the soonest in which all previous articles designed for the delayed issue shall be published.

KWA MAWASILIANO TUMIA ANWANI IFUATAYO:

Please address all inquiries regarding subscriptions to the Director and all editorial matters to the Chief Editor,  Kiswahili, at the following address:          

Kiswahili,

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,

S.L.P. 35110,

Dar es Salaam, Tanzania.

Baruapepe: kiswahili1930@udsm.ac.tz; kiswahili.udsm@gmail.com; iks@udsm.ac.tz

Faksi: +255222410343          Simu: +255222410343.

DISCLAIMER 

[Maoni yaliyomo katika Jarida hili ni ya waandishi wa makala, na si lazima yakubaliane na yale ya Wahariri au Taasisi ya Taaluma za Kiswahili].

[The views expressed in this journal are those of the authors and are not necessarily in accord with those of the Editor or the Institute of Kiswahili Studies].