Malengo na Mawanda

Kiswahili ni Jarida linalojadili na kuendeleza masuala yanayohusiana na lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili. Jarida hili linachapishwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jarida la Kiswahili linachapisha makala zinazopitiwa na wasomaji-fiche. Lengo kuu la Jarida ni kukusanya na kusambaza tafiti mbalimbali na mijadala kuhusu lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930, Jarida la Kiswahili linalenga kuibua fikra za kibunifu na kuhamasisha mijadala ya taaluma anuwai zinazohusu dhana, uchambuzi, sera na utendaji kwa ajili ya maendeleo ya lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili. Jarida linakaribisha mijadala kuhusiana na masuala yote ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kielimu yanayohusu maendeleo ya lugha ya Kiswahili.

Jarida linapokea na kuchapisha miswada ya makala inayohusu lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili, sera ya lugha, na mapitio ya vitabu na makala.