Sera

i.   Sera ya Uchapishaji

Jarida halitozi gharama zozote kwa kuchapisha  miswada ya makala iliyokubaliwa. Miswada yote inapaswa kutumwa kwa kutumia mojawapo au anwani zote zifuatazo: kiswahili.udsm@gmail.com, kiswahili1930@udsm.ac.tz.

Baada ya miswada iliyokubaliwa kuchapishwa, waandishi watapewa nakala tepe ya makala zao zilizochapishwa na nakala ngumu ya Jarida lililochapisha makala hizo.

ii.   Sera ya Ubwakuzi

Matini zote zilizowasilishwa huchunguzwa kama zimebwakuliwa kwa kutumia programu ya Turnitin. Ikiwa kiwango cha kufanana kitazidi 20%, mwandishi atapaswa kuupitia tena mswada. Asilimia za ubwakuzi zikikithiri na ikithibitika kuwa mswada umebwakua matini za watu wengine, mswada utakataliwa mara moja na mwandishi atapaswa kuandika barua rasmi ya kuomba radhi kwa Kamati ya Uhariri.