Mulika Journal

MULIKA ni jarida la taaluma ya Lugha na Fasihii ya Kiswahili. Lilianzishwa mwaka 1970. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja kati ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki.

Makala haya yanapatikana pia mkondoni kupitia wavuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: http://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj


Kamati ya Uhariri

Dr. E. S. Mosha                                      -             University of Dar es Salaam, Tanzania

Prof. M. Mulokozi                                    -             University of Dar es Salaam, Tanzania

Dr. Mussa Hans                                      -             University of Dar es Salaam, Tanzania

Dr. Lutz Diegner                                      -             University of Humboldt, Germany

Dr. Athumani Ponera                              -             University of Dodoma, Tanzania

Dr. Miriam Kenyani Osore                        -             University of Kenyatta, Kenya


   

 

Washauri wa wahariri


Prof. Cyprean Niyomugabo                    -             University of Rwanda, Rwanda

Prof. Sangai Mohochi                            -             University of Rongo, Kenya

Dr. Abel Mreta                                        -             University of Dar es Salaam, Tanzania

Dr. Joseph Nyehita Maitaria                   -              University of Karatina, Kenya

Dr. Selemani Sewangi                            -             Barasa la Kiswahili la Taifa, Tanzania

Prof. Ipara Odeo                                   -             University of Kibabii, Kenya

Dr. Wael Nabil Ibrahim                           -              University of Al Azhar, Egypt

 

 

 

MAELEKEZO KWA WAANDISHI WA MAKALA

 

Jarida huchapishwa mara moja kwa mwaka.

 

Jarida linapokea Makala yaliyoandikwa kwa Kiswahili TU. Makala yapigwe chapa kwenye karatasi za A4, mistari ikitengwa kwa kipimo cha nafasi mbili. Upande mmoja tu wa karatasi utumiwe.

 

Mwandishi awasilishe kwa Mhariri, nakala tatu za muswada wake, pamoja na nakal tepe iliyowekwa katika mfumo wa kikompyuta katika muundo wa Microsoft WORD.

 

Ukurasa wa kwanza wa Makala uoneshe jina la Makala, jina kamili la mwandishi (au waandishi) wa Makala (Ikiwa ni pamoja na wadhifa wake) na anwani yake.

 

Ukurasa wa pili uoneshe jina la Makala na ufupisho wa Makala (Ikisiri) kwa maneno yasiyozidi 300. Jina la mwandishi lisiandikwe.

 

Unapotaja marejeleo kwenye matini taja jina la mwisho la mwandishi, likifuatiwa katika mabano na tarehe ya chapisho lake na kurasa zilizorejelewa, k.m. Yahya (1983:139). Kwenye orodha ya marejeleo au bibliografia majina ya marejelewa yapangwe kialfabeti.

 

Tanbihi ziwekwe namba na zitumike pale tu inapobidi. Maelezo ya tanbihi yatolewe kwenye ukurasa wa pekee mwisho wa Makala.

 

Makala yatatathiminiwa na walau wasomaji wawili, bila ya wao kujua mwandishi ni nani. Waandishi waepuke kuweka utambulisho wowote katika Makala zao ili  wanaosoma Makala hayo na kuyatathmini wafanye kazi yao kwa uyakinifu. Waandishi ambao Makala yao yatakubaliwa kuchapishwa watapatiwa  NAKALA MOJA YA Jarida lenye Makala yao pamoja na malopoo kumi ya Makala yao.

 

Makala yapelekwe kwa:

 

Mhariri

MULIKA,

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,

S.L.P. 35110,

DAR ES SALAAM, Tanzania

 

E-mail: mulika1973@udsm.ac.tz

nukushi: +255222410343.